Kyelafm Radio

Sauti yako mafanikio yako

KYELA FM ILIVYOSHIRIKI KATIKA KUTOKOMEZA UGONJWA WA KIPINDUPINDU WILAYANI KYELA 2017 KWA KAMPENI YA “TUNZA MAZINGIRA YAKUTUNZE”

Kutokana na wilaya ya kyela kuwa katika changamoto kubwa ya ugonjwa wa kipindupindu ambao kwa kiasi kikubwa umegharimu maisha ya watu kwa wengine kufa na wengine kubakia katika viituo maalum vya kuugulia.

Kutokana na tatizo hilo kyela fm radio iliona umuhimu wa kuanzisha kampeni ya “TUNZA MAZINGIRA YAKUTUNZE” kutokomeza kipindupindu ndani na nje ya wilaya ya kyela kwa kufanya usafi wa mazingira ili kunusuru wananchi hao katika maeneo mbalimbali wilayani kyela.

Kwa kuona umuhimu radio ya jamii kyela fm ilishirikisha taasisi na makampuni ikiwemo Songoro Marine kampuni Tanzu ya ujenzi wa meli nchini Tanzania kutekeleza kikamilifu kampeni hii ya usafi wa mazingira katika vituo vya afya ,zahanati na maeneo ya mikusanyiko kwa kuhamasisha wananchi kujua umuhimu wa kutunza mazingira kuwa na taifa lenye watu wenye afya bora.

katika picha ni baadhi ya maeneo ambayo radio ya jamii kyela fm ilifanya kampeni ya “Tunza mazingira yakutunze 2017” kwa kufanya usafi wa mazingira ulioshirikisha wafanyakazi wa kituo hiki na wananchi wa maeneo husika.

Mfanyakazi wa kyela fm James Mwakyembe akiwa katika zoezi la usafi kwenye kampeni ya Tunza Mazingira yakutunze katika eneo la soko la Kandete – Mwakaleli ndani ya Halmashauri ya Busokelo Wilayani Rungwe.
Baadhi ya wafanyakazi Wa Kyela FM wakiwa katika usafi kupitia kampeni ya “Tunza mazingira yakutunze” katika kituo cha Afya Njisi kata ya Njisi wilayani kyela
Mfanyakazi wa kyela FM Elizabeth Asajile akiwa katika kampeni ya usafi ya “Tunza Mazingiya yakutunze yakutunze” katika eneo la Kituo Cha afya Njisi

Meneja wa Kyela Fm Masoud Maulid na baadhi ya wafanyakazi wakikabidhi Misaada ya wagonjwa kwa Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya busokelo katika kituo cha Afya mwakaleli – Halmashauri ya Busokelo