Kyelafm Radio

Sauti yako mafanikio yako

MAFURIKO KYELA 2014 YALIVYOATHIRI SHUGHULI ZA KIJAMII

Adha ya mafuriko ni miongoni mwa majanga ya asili yanaoikumba wilaya ya kyela mara kwa mara. Hii ni kutokana na sababu mbalimbali huku sababu za kijiografia zikichangia kwa kiwango kikubwa.

Mwaka 2014 ni mwaka ambao hautasahaulika katika kumbukumbu za wanakyela wengi, Ni baada ya wilaya ya kyela kukumbwa na mafuriko makubwa ambayo yalileta adha kubwa kwa wakazi wa kyela.

Ilikuwa kipindi cha Mvua za masika katika mikoa ya nyanda ya juu kusini mwa Tanzania mwezi Machi na Mei, Kutokana na Jiografia ya wilaya ya kyela kuwa katika bonde la ziwa nyasa, Mvua hizo ziliathiri kwa kiasi kikubwa mazingira ya wilaya yote kwa ujumla kutokana na mafuriko yaliyoikumba wilaya hii.

Redio ya jamii Kyela Fm ilihusika kwa kiasi kikubwa sana katika kuhabarisha jamii ya wanakyela kutokana na mafuriko hayo juu ya kutoa misaada kwa wahanga wa mafuriko hayo. Pia kyela fm ilikuwa kama kituo cha kukusanyia iliyotolewa na wadau mbalimbali kwa ajili ya wahanga wa mafuriko hayo.

Baadhi ya matukio katika Picha yanaonesha madhara yaliyojitokeza kutokana na mafuriko hayo na namna Redio ya jamii Kyela Fm ilivyoshiriki katika kuhabarisha na kupaza sauti za waathirika wa mafuriko na kukusanya Misaada kutoka kwa wadau mbali mbali.

Muonekano wa Nyumba iliyokumbwa na Mafuliko eneo la Tenende nje kidogo ya mji wa kyela

Mwandishi wa Habari Msuli Mwaijengo akihojiana na Mhanga wa mafuliko
Mkuu wa wilaya ya kyela Magreth Malenga akipokea misaada iliyotolewa na wadau mbalimbali baada ya kuhamasishwa na Redio KYELA FM
Baadhi ya wafanyakazi wa Kyela fm Radio wakipokea misaada kwa ajili ya wahanga wa mafuriko iliyo tolewa na wadua baada ya kuhamasika na kyela fm radio wakati wa mafuriko
Gari la Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya kyela Clemence Kasongo likiwa limebeba baadhi ya Wandishi wa Habari wa kyela FM likiwa limekwama kwenye maji Kata ya Katumbasongwe.