Kyelafm Radio

Sauti yako mafanikio yako

MGOMBEA UDIWANI (CCM) KATA YA KYELA APITA BILA KUPINGWA

Msimamizi wa uchanguzi  na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya kyela Lucy Mganga amemtangaza Andrea Ngayocha wa chama cha mapinduzi kupita bila kupingwa katika nafasi ya udiwani kata ya kyela mjini baada ya wagombea wengine kutokurudisha fomu.

Msimamizi huyo amesema katika mchakato wa uchaguzi hadi siku ya kurudisha fomu ni mgombea mmoja pekee kupitia chama cha mapinduzi ccm aliyerudisha fomu hivyo kwa mujibu wa sheria za uchaguzi mgombea Andrea Ngayocha ametangazwa kuwa mshindi wa kiti cha udiwani bila kupingwa.

 

Kwa upande wake mgombea aliyepita bila kupingwa Andrea Ngayocha amesema kupita bila kupingwa kunatokana na kazi zinazofanywa na chama cha mapinduzi ccm kwa wananchi katika sekta mbalimbali hivyo vyama vingine vimeunga mkono kwa kutosimamisha mgombea ili chama tawala kiendelee kuwatumikia wananchi.

Nae Mgombea kupitia chama cha CUF Haki Matola ambaye alichukua fomu na kushindwa kurudisha amesema kufanyika kwa uchaguzi mdogo ni ufajaji wa fedha za wananchi huku katibu mwenezi wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema Donald Mwaisango amebainisha sababu kwanini chama hicho hakikushiriki kwenye uchaguzi huo.

Uchaguzi wa kata ya kyela mjini umefanyika baada ya aliyekuwa diwani wa kata hiyo Azory Sanga kupitia chama cha demokrasia na maendeleo chadema kufariki dunia mwanzoni mwa mwezi wa tatu mwaka elfu mbili na kumi na tisa.