Kyelafm Radio

Sauti yako mafanikio yako

WATOTO NI TAIFA LA BAADAE TUWASAIDIE.

katika kuhakikisha jamii inafanya jitihada ili kuwawezesha watoto walio na ulemavu na shida mbalimbali zinazo pelekea kushindwa kupata mahitaji madogomadogo.

kyela fm Radio imekuwa mstali wa mbele kuhakikisha jamii inachangia michango mbalimbali ili kuwasaidia vijana na watoto kupata pesa za kukidhi mahitaji yao japo kwa kidogo kinacho patikana.

pichani ni mtoto BARAKA mlemavu wa jicho akiwa amechangiwa kiasi kidogo cha shilingi laki tatu kumi na saba na miatatu, (317,300/=Tsh),Meneja wa kyela fm Radio Ndg Masoud Maulidi pamoja na katibu wa wadau Kyela fm Radio Tumpe Gidion wakiwasilisha kiasi kilicho patikana kwa mtoto mlengwa.

CHANGAMOTO

1; kutokuwa na miradi wezeshi ya kusaidia vijana wapate misaada ya kuwasaidia wapate Elimu

2;Idadi kubwa ya wahitaji

3;Uelewa mdogo kwenye jamii katika kushiriki kutoa misaada.